Somo la tatu. USHIRIKA KIUFUPI (Fellowship - Briefly)

Ni furaha iliyoje tukikaa pamoja katika amani ya Kristo! Tuna amani moyoni na akili ambayo hupita fahamu zote za mwanadamu na tunamjua yeye kama aliyefufuka. Tunaamini kwa Mungu kupitia hili Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Hili huliangalia na kulifundisha. Tuliungana na Mungu kupitia amani aliyotushindia Yesu pale Kalvari. Sio tu tunaunganika na Mungu kwa imani katika Kristo, bali tunaungana pamoja na mwingine katika kanisa kwa imani yetu ya kila siku. Kama vile tunavyo imani kwa Mungu. Hivyo inatupasa kuwa na uhisano wa Amani na wengine katika kanisa lake. Kama Paulo asemanvyo, Tunapaswa kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani (waefeso 4:3).

Umoja huu tulio nao katika roho huonyesha kwamba sisi kama kanisa kukubaliana na kufundisha neno lake katika usafi na ukweli wake. Tumeunda mwili wa kanisa wanaoonekana ili kutenda pamoja kwa ajili yake katika ufalme wake. Umoja wetu unalemea juu ya neno safi la Mungu. Hatutastahili mafundisho yoyote ya uongo au walimu wa uongo tunatafuta kusimama imara katika Roho moja kwa moyo mmoja mkishindania imani ya injili (Filip 1:27). Umoja sio kulemea katika makubaliano juu ya kila neno la Mungu hufundisha, siyo andiko la kweli la umoja. Zaidi na zaidi tena, neno hutuambia kwamba kwa kila kikundi cha wakristo kutenda pamoja kwa ajili yake, kumwabudu pamoja na kufanya kazi yoyote ya dini pamoja, lazima yawepo makubaliano juu ya neno lake lifundishavyo. “Nawasihi ndugu zangu, kwa jina la Bwana wetu Yesu kristo, kwamba nyote mnene mamoja wala pasiwe kwenu faraka bali mhitimu katika nia moja na shauri moja” (Icor 1:10). Umoja wetu chini ya Mungu katika mwili wetu wa kanisa umelemewa juu ya kuyakubali yote ambayo neno la Mungu hufundisha na si kwa kuongeza na kupunguza.

Mafundisho yetu sahihi ni kwamba tunakubaliana na kila neno linalosemwa na hata kutendea kazi ushirika wa dini katika yote miundo yake tofauti tofauti. Ibada, maombi, mafundisho na mahubiri, utoaji, kazi ya kanisa.

Hatuwezi kuwaminia fundisho la uongo ndani ya kanisa letu kwa sababu Mungu husema hatuwezi. Hata kama ni fundisho moja la uongo haliwezi kuruhusiwa kama vile Paulo asemavyo, “chachu kidogo huchachua donge nzima” (wagal 5:9). Bwana wetu alifundisha kwamba sisi ni kuendelea katika neno lake na kujihadhari na walimu wa uongo. Sawa sawa kama tusingeweza kuvumilia mafundisho ya uongo. Hivyo hatuwezi wote ambao hufundisha uongo.

Ni sawa kama haturuhusu fundisho la uongo au walimu wa uongo kufundisha ndani ya kanisa letu, hivyo hatupaswi kutendea kazi ushirika wa dini na walimu wa uongo na makanisa yao na hata mifumo yao. Andiko husema wazi katika Wakorinth, “ndugu zangu nawasihi waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza mkajiepusha nao kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe na kwa maneno laini nayo kujipendekeza wakijidanganya mioyo ya watu wanyoofu (Rum 16:17). Lakini kulitokea manabii wa uongo katika wale watu kama vile kwenu kutakavyokuwepo walimu wa uongo watakaoingiza kwa werevu na uzushi (IIpet 2:1). Inatupasa tuombe tu na wale ambao tunakubaliana nao, hatuwezi kushiriki wahubiri wetu na makanisa mengine ambayo yana baadhi ya makosa.

Tunatoa matoleo yetu kwa ajili ya mafundisho ya neno safi na yote katika hili na siyo kwa kuenea au kuachilia makosa. Tunajifunza neno pamoja kwa sababu tunakubaliwa hasa. Tunapiga magoti pamoja kupokea mwili wa Bwana na damu kwa kuwa tunaungana katika ukiri wetu wa imani. Hatupokei meza ya Bwana katika makanisa mengine kwa kuwa hatukubaliani na mafundisho yao. Haijalishi kosa dogo kiasi gani bali bado ni kosa na unaweza kula kama saratani iliyoachwa peke yake. Tunalishikilia juu neno la Mungu na utimilifu wake kama hazina tuliyofundishwa na kujifunza. Kuumbuka jinsi gani kosa lilivyo hatari na kwa hiyo ndiyo maana hatupaswi kuliachilia kama ukichanganya maji ya tope na maji safi hutaendelea tena kunywa? Ni yale yenye lishe kamili na masafi au yale ya matope. Hata kama ukichanganya na maji madogo ya matope na masafi, maji hayatabakia masafi tena. Pia shauri lote la neno la Mungu ni kufundishwa na siyo baadhi au sehemu tuna wajibu wa kusema kile kilicho halali na kilicho kibaya kutoka neno la Mungu. Tusihukumu, ni neno pekee (lenyewe) huhukumu kuchagua kutoka katika neno.