Somo la kwanza . NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA (The Position of Women in the Church
Mwanamke anaweza kushika ofisi katika kanisa? Mwanamke anaweza kuwa mhubiri katika kusanyiko la Kikristo? Leo katika nakala hii kama zilivyonyingi, kanisa limekuwa likisikiliza ulimwengu zaidi kuliko kulisikiza neno. Hebu natusikilize kutoka kwa neno safi la Mungu. Litatupa majibu kwa maswali yote ambayo yatajibiwa katika sehemu hii ya milele. Na mwili wetu wa kanisa la Kilutheri liweza kupenya kwa hilo neno safi kiuaminifu.
UUMBAJI WA MWANAMUME NA MWANAMKE.
Kwa kufahamu ubora kabisa wa uhusiano wa mwanamume na mwanamume na mwanamke ni muhimu kurejea mwanzo wakati Mungu aliwaumba katika siku ya sita ya muumbaji. Mungu alimumba Adamu kwanza na baadaye, Eva, mwanamke. “Hivyo Bwana Mungu akasababisha usingizi mzito kwa mwanamume, na alipokuwa amelala alichukua ubavu wake na kufunika mahali aliouchukua kwa nyama, na ubavu ambao aliolewa ameuchukua kwa mwanamume, akaufanya mwanamke na kumletea mwanamume” (Mwanzo 2:21-22).
Mwamke aliumbwa ili awe msaidizi anayemfaa mwanamume (Adamu), Eva alifanywa kutoka katika ubavu wake Adam kudhihirisha jinsi anavyopaswa kuwa pembeni ya mwanamume kama msaidizi. Mwanamume ni kichwa cha familia pamoja na mwanamke kama msaidizi wake. Baada ya kuanguka katika dhambi, Mungu alisema kwa uhusiano wa mwanamume na mwanamke, “mwanamume atakutawala” akirejea kwa mwanamke (3:16 mwanzo). Hii ni mpangilio wa Kiungu kutoka mwanzo. Mwanamume alikuwa ni kichwa cha nyumba yake, alipaswa kumtawala mkewe. Mwanamke alipaswa kujinyenyekeza kwa mume wake na kuwa msaidizi anayefaa.
NAFASI YA MWANAMUME NA MWANAMKE KATIKA UHUSIANO NA MUNGU.
Mwanamume na mwanamke pamoja husimama na kulaumiwa na sheria ya Mungu kuwa ni wakosaji. Wote wamefanya dhambi nakupungukiwa na utukufu wa Mungu, hii inamaanisha mwanamume na mwanamke. Hakuna hata mmoja afanyaye mema hata mmoja, japo mwanamume au mwanamke. Wote wamezaliwa katika hali ya dhambi na kusababisha wao kugeuka mbali na Mungu. Soma warumi sura ya tatu. Hivyo wote mwanamume na mwanamke ni wakosaji wanahitaji wokovu.Yesu alikuja kuwaokoa wakosaji, yaani pamoja na wanamme na mwanamke. Yesu ni mwokozi wa watu wote. Alilipa fidia ya dhambi zote. Hivyo dhambi zao zote zimelipwa pale Kalivari. Sasa Mungu huwaita wote kila mahali kutubu na kuamini. Wakati huo wanaume na wanawake ni wenye dhambi na wote wanahitaji msamaha sawa na siyo misamaha tofauti. Mwanamume na mwanamke wana majukumu tofauti katika maisha. Hakuna mmoja wapo angelaumu kwamba jukumu la kuzaa watoto limepewa wanawake na siyo wanaume. Hilo ni rahisi kuwa kwa wote wana jinsia tofauti. Mwanamume kwa ujumla nguvu za kimwili ni imara kuliko mwanamke. Na hivyo pia wamepewa na Mungu majukumu tofauti katika maisha.
MWANAMUME NA MWANAMKE KATIKA FAMILIA.
Mnyenyekeane katika kicho cha Kristo (Waefeso 5:21) kila mmoja wenu katika sehemu yake ya maisha iwe kunyenyekeana katika njia ambayo Mungu huamuru. Ni Mungu ambaye aliyeanzisha ndoa na familia wakati alipompa mwanamume Eva katika bustani ya Edeni. Ni Mungu aliyepanga jinsi watu hawa wawili wanavyo paswa kuwa katika familia.
Wake, watiini waume zenu kama kwa Bwana. Kwa kuwa Mume ni kichwa cha mke kama kristo alivyo kichwa cha kanisa, mwili wake, na yeye mwenyewe ni mwokozi kama kanisa linavyomtii kristo, hivyo wake nao wawatii waume zao kwa kila kitu. (Waefeso 5:22-24) Tunaweza mara chache kufananisha kwamba kanisa linapashwa kuasi juu ya Bwana wake. Hivyo pia wake wanapashwa kuwa watiifu na sio kuwaasi waume zao. Kanisa husikiliza na kutii Bwana wake. Hivyo hivyo na mke anapaswa hivyo kwa mmewe. Mke anaweza kutokubaliana na yote mme wake anayofanya au anayosema. Lakini isipokuwa kutenda dhambi na kuweza kumwingiza mwanamke kutenda dhambi, wanamke anapaswa kutii yote isipokuwa dhambi.
- Waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyo lipenda kanisa na kujitoa yeye mwenyewe kwa kanisa
- …………. Hata hivyo waume imewapasa kupenda wake zenu kama miili yenu wenyewe. Anayempenda mkewe anajipenda yeye mwenyewe …………. “(Waefeso 5:25-28) kama Mungu alivyolipenda kanisa kwa upande mkuu, hivyo waume wajitoe kwa wake zao …………… “wapendeni wake zenu na msiwe wakali kwao” Wagal 3:19” ……………….. kaeni na wake zenu kwa akili, na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu ………………..” (I petro 3.7) kutoka katika vifungu hivi hatuwezi kuona kuwa mwanaume amekuwa katili kwa mke wake. Anapaswa kumtawala, kwa upendo. Kwa kila mmoja amepewa kazi, katika familia. “……………….kila mmoja ampende mkewe kama yeye mwenyewe, na mke aone kwamba amheshimu mmewe (Efeso 5:33).
MWANAMUME NA MWAMKE KATIKA KANISA
Kama Mungu alivyoanzisha familia, hivyo pia alianzisha kanisa lake duniani. Kama vile alivyolielekeza na majukumu kwa wote katika familia, hivyo na pia wote walioko Kanisani. Kama ilivyo mwanamume ni kichwa cha nyumba na juu ya mke, hivyo kristo ni kichwa cha kanisa. Askofu, shemasi na mzee ni ofisi katika kanisa zilizotajwa katika agano jipya. Kwa kila mmoja anatakiwa awe “mme wa mke mmoja” ( I Tim 3:2,3:12 ,Tito 1:6). Ni kwamba Mungu katika ufahamu wake wa mbele alijua kwamba mwanamke angejaribu katika siku hizi za mwisho kwa kugeuza mpangilio wa Kimungu. Kuwa kiongozi, mhubiri, mamlaka katika kanisa juu ya wanaume halikadhalika wanawake na waoto kumaanisha kuwa kichwa cha kanisa. Kichwa hicho lazima kiwe ni mwanamume kuongoza kanisa, kama vile ilivyo mwanamume ni kichwa cha nyumba.
“mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu” (I Timotheo 2:11-12). Imeamriwa kwamba mwanamke afundishe watoto na hata wanawake wengine, lakini kwao kufundisha wanaume katika kanisa ni kukiuka mpangalio wa kimungu. Mamlaka katika kanisa yamekabidhiwa kwa wanaume. Kanuni hii imewekwa vizuri katika vifungu tulivyokwisha kuvitaja katika Timotheo na Tito. Kama mwanamke angekuwa mhubiri au mchungaji, nani angefanyia mazoezi au utendaji mamlaka juu ya wanaume? Kama wanawake wangeruhusiwa kufanya maamuzi kwa kusanyiko badala ya wanaume, hivyo wanatendea kazi mamlaka juu ya wanaume. Kama mwanamke wangeruhusiwa kufanya maamuzi kwa kusanyiko badala ya wanaume, hivyo wanatendea kazi mamlaka juu ya wanaume. Kama mwanamke akifanya au kuongoza kujifunza, hivyo huyo mwanamke anatawala mamlaka juu ya wanaume katika kanisa. Kuwa aina ya mtawala juu ya wanaume ni kutendea mamlaka juu ya wanaume ambapo sio mpangilio wa kimungu. Kama tunafuata fikira zetu wenyewe, hivyo tunatenda dhambi. Katika kusanyiko la Korintho Paulo aliweka kanuni hii ambayo aliielezea kwa Timotheo kwa maana Mungu sio Mungu wa machafuko bali wa amani. Kama ilivyo kwa makanisa yote ya watakatifu, wanawake wanyamaze kimya katka kanisa. Kwa maana hawaruhusiwi kuongea, bali wanapaswa kuwa chini (kutii) kama hata sheria isemavyo. Kama kuna chochote anatamani kujua, na amulize mmewe nyumbani. Kwa maana ni aibu kwa mwanamke kunena katka kanisa. (Ikor 14:33-36) hii lazima iwe hakika ya msemo mgumu wa Paul. “Natuseme nini?” kanuni kama ilivyotiwa kwa Wakorintho ilikua kali sana. Kusanyiko lilikuwa katika mchanganyiko wa lugha, kugawanya sehemu ya Roho, na wanawake kwa ujasiri wakichangia katika machafuko kwa kuchukua mamlaka juu ya wanaume katika ibada za wazi wanaume walifundishana kuhubiri. Wanawake wa Korintho na sehemu hawakuwa wanyenyekevu, na kufanya mabishano ya wazi na wanaume wahubiri na walimu.
VIPI LEO?
Wanawake wanaweza kushikilia ofisi katika kanisa kama mhubiri au mchungaji? Neno la Mungu linasema hapana. Wanawake wanaweza kushikilia ofisi katika kanisa ambapo wangechukua majukumu ya shughuli za kikanisa na kuwatawala wanaume? Neno la Mungu linasema hapana. Kama wanawake wanafundisha wanaruhusiwa kufundisha wanawake wengine na watoto hilo limeamriwa. Mpango wa Kimungu una madhumuni hata kama wengine hawatakubaliana nao. Mpango au mfumo wa Kimungu ni kwa wanaume kuongoza katika kanisa kama vile walivyo kichwa cha nyumba. Kama kuna wale wanaosema kuwa Paulo maandiko haya hayatuhusu sisi wa kizazi hichi, lazima watuambie kwa nini. Kulikuwa na desturi kai ya Wakorintho ambazo hatupaswi kulishikilia leo, kweli inatosha. Lakini mfumo wa kimungu katika nyumba na katika kanisa inafungumana na vizazi vyote. Ni mwokozi mwenye upendo ambaye neon lake hutuambia ukweli. Hebu na tusikilize neno la Mungu nasiyo mawazo ya wanadamu wenye dhambi katika ulimwengu huu unaobadilika, ambapo kuna mawazo ambayo yanapingana na kinyume na Bwana wetu upendo.
Kwa kuhitimisha, sisi kama walutheri tunaenda sambamba na neno la Mungu na siyo tunalipita neno (uf 22:18-19). Kwa mfano hatusemi kuwa wanawake hawawezi kujihusisha na shughuli au siasa katika serikali. Maandiko hayasemi kuhusu hilo, hivyo nasi tunanyamaza kimya pale Biblia imenyamanya kimya.