Somo la sita. MEZA YA BWANA (Communion)
Utangulizi.
Andiko lina maelezo mengi ambayo ni kweli iliyo kama uongo ambayo wapo nyuma ya ufahamu wa mwanadamu. Kama kitu cha kweli ilivyo ya uongo hubeba vitu vya kukanusha kwa kila moja kulingana na sababu ya mwanadamu lazima tuamini juu ya ufahamu wa Mungu katika vitu vya Kiroho na kuamini neno lake kwa imani. Imani inauwezo wa kushika kitu ambacho kipo juu ya sababu ya mwanadamu imani hukubali jinsi neno linavyofunua. Tunaamini katika utatu, nafsi tatu katika Mungu mmoja hii ni fumbo na siri kukubalika kwa imani tunaamini Yesu ni Mungu na ni mwanachama hivyo ana asili mbili. Sababu yetu haiwezi kushika kwamba ndani ya nafsi moja kuwe na asili ya kiuanadamu na asili ya Kimungu. Bado hili ni hasa jinsi ilivyo katika nafsi ya Yesu. Kuhoji kunasema “haiwezekani, ingawa imani kusema’ naamini”
Tunakubali kwa imani kwamba neno la Mungu hufundisha katika ushirika tuna siri na fumbo la maneno. Hili fundsho la neno kale yatupasa tuamini. Tabia yetu inapaswa iwe kama ile yakijana Samweli, “sema Bwana kwa maana mtumishi wako anasikia” hebu nauwe tayari kusikia na kukubali kwa kuamini miongoni.
MANENO YA KRISTO
Fundisho juu ya meza ya Bwana linapatikana katika Mt 26:26-29 mk 14:22-25 lk 22:19-22 Ikor 11:23-30 10:14-22. kutokana na hizi rejea, tunamsikia bwana wetu kwa wazi akisema juu ya mkate, “huu ndio mwili wangu” na juu ya mvinyo, “hii ni damu yangu japo aliwaambia wanafunzi wake kula mkate na kukinyea kikombe. Anarejea mambo manne ya msingi yaliyopo katika meza ya Bwana: mkate na mvinyo, mwili wake na damu yake. Tunasema kwamba kuna mambo ya Kimbingu yaliyo wakilisha wakati tunaposhiriki meza ya Bwana.
Wakati Bwana wetu hutuambia kwamba katika meza yake tunapokea mwili wake uliotolewa kwa ajili yetu na damu yake iliyomwagika kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi, hivyo tunafahamu kwamba katika tendo hili la Kiungu la Bwana huwapa washirika uhakika wa msamaha wa dhambi kama ilivyofanya injili katika neno. Wakati tunapolifanya hili kwa kumkumbuka yeye tunakumbuka kifo chake, kuwa na faraja ya msamaha wa dhambi. Mara kwa mara tunapokula na kunywa, tunatangaza imani yetu katika kazi yake ya kulipa kosa kwa ajili ya wokovu wetu.
ANDIKO HUTAFISIRI ANDIKO
Tunaamini dhabiti kwamba Biblia hujieleza yenyewe kwetu. Kuelewa kwa imani baadhi ya misemo migumu, ni rahisi jifunze zaidi kuna maziwa katika neno na kama chakula katika neno lakini zaidi ya yote “kwanza ya yote lazima ufahamu hili kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu Fulani tu (II pet 1:20).
Pamoja na maneno ya ushirika tunayatumepewa. Tunayaelewa kulingana na mazingira yake. Na tunayoelewa kulingana na marejesho ya msalaba na vifungu vingine juu ya ushirika. Katika asili tunachukua maneno katika uhalisi wake, maana ya asili isipokuwa maziwa au vifungu vingine kueleza maneno katika mtazamo wa lugha ya mfano.
KUNA KITU CHA ZIDA KULIKO MKATE TU NA MVINYO HAPA.
Paulo anasema katika I kor 11:28 kwamba kama mtu akishiriki kwa njia isiyopaswa bila kupambana mwili wa Bwana na damu atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana mtu hashtakiwi katika mkate na mvinyo wa kidunia hilo lingiweza kuwa ni ujinga hapana kitu kingine kikubwa kuliko mkate na mvinyo hapa au Paulo hangelinena hivyo. Paulo anasema ambaye hataweza kupambanua mwili na damu na ambaye yeyote bado kula na kunywa “hula na kunywa hukumu yake mwenyewe (I kor 11:29). Kauli kali muone juu ya hili jambo kama ni mkate tu na mvinyo katika kusanyiko la Korintho. Paul anaeleza jinsi gani hukumu hujionyesha yenyewe “kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu na watu kadha wa kadha wameleta(kufa) I kor 11:30. Pale K orintho kibinafsi palitokea ushirika ambao hawa kutubu dhambi zao hili liliwafanya wawe wasiostahili walichulia ushirika kwa dharau na hawakutumaini katika msamaha wa dhambi kupitia mwili wa kusto na damu hili lilileta hukumu juu yao katika I kor 10 Paulo hutuambia kwamba katika kushiriki mkate ni ushirika katika mwili wa Kristo na kule kushiriki kikombe ni ushirika katika damu ya Kristo” linahitajika sana wakati njia ya siri tuna poshiriki mwili wa Kristo na damu yake na mkate na mvinyo kwa ondoleo la dhambi?
NGUVU KATIKA NENO.
Ni rahisi mvinyo na mkate hadi tunashiriki kusikia na kuamini maneno ya Kristo kadri tunavyoshiriki inakuwa maana ambayo Mungu hutia nguvu imani zetu kutuhakikishia kuwa tuna neema ya Mungu katika Kristo. Wakati tukisikia neno la Mungu pekee hivyo Roho mtakatifu hufanyakazi katika moyo kadhalika pia katika ushirika kadri tunasikia neno la mungu na kushika, Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yetu. Waprotestaint wengi husema katika ushirika hakua msamaha wa dhambi wanasema kwamba mwili wa Kristo na damu haviwezi kuwakilisha kwa kukuwa kama ni hivyo yawezekana kuwa wala watu (canni balism) watu kuwa hawaelewi nguvu ya neno la Mungu.